×

Steve Nyerere Alikoroga Ndoa ya Joti

Joti na mkewe siku ya ndoa yao.

Muigizaji na mchekeshaji Steve Mengere maarufu kama Steve Nyerere amelikoroga katika ndoa ya mchekeshaji mwenzake, Lucas Mhuvile ‘Joti’ kufuatia ‘comment’ yake kumpongeza kwa tukio hilo kubwa maishani mwake.

Katika pongezi hizo, Steve Nyerere alimpongeza Joti huku akitoa maneno ambayo yalionekana kama ni kijembe kwa mzazi mwenzake na Joti, Merisa Bushoke aliyekereka na kuamua kumjibu vibaya.

Steve baada ya kuhudhuria kwenye hafla ya Joti alipiga picha na kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alimsifia kwa kufanya maamuzi magumu ya kumuoa mwanamke ambaye si mzazi mwenzake, lakini kwenye maneno hayo, alimpongeza mtoto wa Joti kwa kupata mama bora huku akimwambia kuwa ule usemi wa mama wa kambo si mama wakati mwingine si wa kweli.

Maneno hayo yalimkera mzazi wa mtoto wa Joti ambaye naye aliamua kumjibu na kumtahadharisha kuwa asijione mdogo wakati yeye ni mkubwa kwani maneno aliyotumia hayakuwa sahihi.

Steve Nyerere.

Mtandaoni, Merisa aliandika:

“Nahitaji kusema hivi, huyu ni mtoto wangu na mimi ndo niliyemzaa, hata mama awe chizi, taahira, mjinga ndo mama ake na haitokuja kutokea yoyote ukamfananisha na upendo wa mama ake kwa hiyo sitaki maneno na mtu yoyote kama unataka kupongeza kitu kizuri kilichofanyika tumia maneno yasio mhusisha mwanangu, nadhani umenielewa na maana yako nini kuongea ulichoongea, sijapenda wewe ni mkubwa jielewe, ufupi usikufanye ukajiona bado mdogo.”

HARUSI YA JOTI: Aendeleza Vituko Hadi Kanisani!

Baada ya majibu hayo ambapo Merisa alimtagi Steve Nyerere ili aone, Risasi Jumatano lilimtafuta mchekeshaji huyo ambaye alicheka na kuomba Merisa aachwe.

“Hahaha achana naye bwana,” alisema Steve ambaye baadaye alifuta ujumbe alioandika kwenye safu yake kuhusu ishu hiyo. Merisa aliposakwa kwa njia ya simu ili aeleze kilichomkera zaidi simu yake iliita bila kupokelewa.

Na Mwandishi wetu, Risasi Mchanganyiko | DAR ES SALAAM

Leave a Comment