MCHUNGAJI mmoja wa nchini Ghana, Sylvester Ofori (35), ametiwa mbaroni nchini Marekani anakoishi baada ya kumuua mkewe, Barbara Tommey (27).
Amemuua kwa kumfyatulia risasi saba nje mbele ya ofisi anazofanyia kazi mkewe huyo ambapo kamera za CCTV zimenasa tukio hilo ingawa sababu za kumuua mkewe hazijajulikana.
Kwa mujibu wa taarifa, baadhi ya ndugu wa mke huyo walishamshawishi ndugu yao huyo aachane na mwanamme huyo baada ya kugundua mke alikuwa ananyanyaswa muda mrefu na mume huyo lakini mwanadada huyo akawa anavumilia kuona pengine mume angebadilika.
Mbali na kamera hizo, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Lisa aliyeshuhudia pia tukio la mauaji hayo, amesema lilikuwa tukio la kinyama kwake kushuhudia kwani lilimshutua mno, akiongeza kwamba Barbara alikuwa mtu mkarimu aliyekuwa akihudumia watu vizuri ofisini kwake.

