×

Ndugai Atoa ‘Bonus’, Kisa Magufuli – Video

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amewaomba wananchi wa Urambo kumpa kura za kishindo mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli, na mgombea ubunge wa jimbo hilo, Magreth Sitta, akisema kwa kufanya hivyo watapata nyongeza ya mbunge wa viti maalum.

 

Ndugai ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 21, 2020, katika mkutano wa kampeni za CCM, wakati akimuombea kura Magufuli  na mgombea ubunge wa jimbo  hilo, Margareth Sitta.

 

“Sisi wa CCM tunaomba kura tatu ya kwanza ya rais, wabunge na madiwani na hapa Urambo namuombea Mama Margareth Sitta na ukipiga kura kwa Magufuli na Mama Sitta kwa Urambo hapa unapata ‘bonus’ kwa sababu mtampata mbunge wa viti maalum anaitwa Jackline”, amesema Ndugai.

 

Aidha ameongeza kuwa, “Tusichague wapinzani kwa sababu tatizo lao ni kupinga kila kitu, Rais Magufuli akitaka kujenga reli wanapinga, akitaka kujenga barabara na kusambaza umeme na akitaka kutoa maji Ziwa Victoria kuleta Urambo wanapinga sasa mtu wa namna hiyo wa nini?”

Leave a Comment