×

Kikongwe (84) Jela kwa Kugushi Hati

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemhukumu mzee wa miaka 84, Ally Baruhani Macho,  miaka minne  jela kwa kosa la kugushi hati ya kiwanja.

 

Hukumu hiyo imetolewa hii jana Septemba 21, 2020 na Hakimu Mkazi Rashidi Chaungu ambapo upande wa jamhuri ulikuwa na jumla ya mashahidi watano na upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi wanne.

 

Hakimu Chaungu amesema kuwa ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri dhidi ya shtakiwa.

 

Aidha upande wa jamhuri uliowakilishwa na mawakili Ashura Mzava na Kija Elias umeeleza nia ya kukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo iliyotolewa kwa mshitakiwa.

 

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo na kuwasilisha nyaraka za uongo ambapo aligushi hati ya kiwanja Plot namba 894 block G kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam, mali ya Haidari Kavira.

Leave a Comment