UONGOZI wa Klabu ya Yanga leo Oktoba 3,2020 umefikia makubaliano ya kumfuta kazi kocha wao mkuu, Zlatko Krmpotic raia wa Serbia aliyechukua mikoba ya Luc Eymael.
Zlatko amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara ambapo katika mechi hizo ameshinda mechi nne na kulazimisha sare moja ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons.

