×

Breaking: Watano Wafariki Ajali ya Daladala na Lori Dar – Video

WATU watano wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani iliyohusisha daladala na lori la mchanga katika eneo la Chang’ombe jijini Dar es Salaam iliyotokea alfajiri ya leo Jumatatu, Oktoba 5, 2020.

 

 

 

Kamanda wa Polisi Temeke jijini Dar es Salaam, Amon Kakwale,  na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba jeshi hilo linaendelea na uchunguzi  kuhusu chanzo cha ajali hiyo.

Amesema ajali hiyo imetokea leo alfajiri na imesababishwa na dereva wa daladala kupita wakati taa nyekundu zinawaka. Daladala hiyo hufanya safari zake  maeneo ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema waliokufa ni pamoja na wanaume watatu na wanawake wawili waliokufa papo hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, chanjo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kwa kushindwa kuzingatia taa za barabarani.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ambao wengine walikuwa sehemu ya abiria kwenye basi hilo lililokuwa linatoka Temeke kwenda Muhimbili, wamesema pamoja na kumsisitiza dereva kuzingatia alama hizo, alipuuza kabla ya basi hilo kugongana na lori kwenye makutano.

Daktari Meshack Shimwela, Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Temeke amesema kuwa wengine wanne waliojeruhiwa walipata huduma ya kwanza na tayari wamepelekwa hospitali ya Muhimbili kwa tiba zaidi huku wengine wakiendelea kupata matibabu katika hospitali ya Temeke.

Updates
DAR ES SALAAM 05.10.2020
Mpaka sasa Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea majeruhi watano kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke waliopata ajali leo asubuhi  05.10.2020 eneo la Chang’ombe-Temeke.
1. William Paul Akida (Me-42)
2. Jina halijafahamika (Me-32)
3. Jina halijafahamika (Me-20)
4. Alicia Teophil (Ke-25)
5. Valentino Lucas (Ke-29)
Wanaendelea na matibabu. Haya yamethibithishwa na Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment