×

Shigongo Afariji Familia Mbili Zilizopoteza Ndugu Zao

MGOMBEA ubunge Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James, licha ya kuwa na ratiba ya kampeni katika kata na vijiji tofauti, amezitembelea familia mbili zilizopata msiba kwa kufiwa na ndugu zao katika vijiji  vya Nyakaliro na Lumeya na kuwafariji wafia, ndugu, jamaa na marafiki wa familia hizo.

Shigongo ambaye siku zote amekuwa mtu mnyenyekevu, mpenda watu na mwenye huruma, amekuwa akionyesha upendo mkubwa kwa wananchi wenzake wa Jimbo la Buchosa na taifa kwa jumla na kujumuika nao katika matatizo mbalimbali.

Shigongo anaendelea na kampeni zake jimboni Buchosa akinadi sera za chama chake cha CCM pamoja kuwaomba ridhaa  wananchi ili wawachague viongozi wa CCM kuanzia kiti cha urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

 

 

 

Leave a Comment