RAIS wa Malawi, Lazarus Chakwera, anatarajiwa kukaa nchini siku tatu ambapo atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Rais John Magufuli, atatembelea bandari ya Dar es Salaam na kuzindua stendi mpya ya kisasa ya mabasi iliyopo Mbezi-Mwisho jijini Dar es Salaam.