NAELEZWA mmiliki wa Kampuni ya GSM, Ghalib Salim Mohamed ameamua kuwanunulia wachezaji wa Yanga vifaa maalum kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.
Yanga inatarajiwa kucheza na Simba, Novemba 7, mwaka huu katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar.
Bosi huyo amenunua vifaa hivyo ikiwa ni zawadi yake kwa wachezaji hao baada kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya tights pea mbili kwa kila mchezaji huku akitumia jumla ya Sh milioni tano, maalum kwa ajili ya vifaa hivyo.
Yanga ina wachezaji 28, katika vifaa hivyo kila mchezaji anatakiwa kupata viatu vya kuchezea KMKM katika mchezo wa kirafiki uliopigwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar.
Mara baada ya mchezo huo, bosi huyo alishauriana na viongozi wa timu hiyo juu ya zawadi yake kabla ya kuamua kutoa pesa ya kununua viatu vya kuchezea pamoja na skin pea moja ambavyo ni Sh 150,000 pamoja na skin tights mbili, kijani na njano huku kila moja ikiwa ni sh elfu 20,000 ambayo kwa wachezaji 28 jumla yake inakuwa ni sh 560,000.
sTORI: Ibrahim Mussa na Abdulghafal Ally
LIVE: RAIS MAGUFULI AKIWEKA JIWE LA MSINGI KITUO KIPYA CHA MABASI MBEZI MWISHO

