MGOMBEA ubunge Jimbo la Buchosa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James, ametumia usafiri wa pikipiki wakati akielekea kwenye kampeni zake, Kata ya Bukokwa leo Alhamisi, Oktoba 8, 2020.
Vijana ambao ni madereva wa bodaboda katika Kijiji cha Bukokwa walingia katika msafara wa Shigongo mpaka eneo la mkutano alipokuwa amepanga kuzungumza na vijana wa kata ya Bukokwa katika Halmashauri ya Buchosa.
Shigongo amewaasa vijana hao kuchagua viongozi bora wanaotokana na CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo yao pamoja na kuzisaidia familia zao.
Kwa upande wao, vijana hao wamesema wanamuunga mkono Shigongo kwa asilimia 100 na kwamba watampigia kura nyingi kwani wanaamini ndiye kiongozi bora atakayewasemea bungeni na atakayeweza kuwasaidia katika harakati zao za kutafuta maendeleo na kuitengeneza Buchosa mpya.
Shigongo anaendelea na kampeni zake jimboni Buchosa akinadi sera za chama chake cha CCM na kuwaomba ridhaa wananchi ili wawachague viongozi wa CCM kuanzia kiti cha urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.


