
Washtakiwa watatu raia wa Liberia na wengine wawili raia wa Nigeria na Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili yote yakiwa niya kuingia nchini bila kibali.
Washtakiwa hao ni Ibrahim Darbey (Liberia),Prince Robart (Liberia), Cream Milton (Liberia), Adewale Oyedeji (Nigeria) na Basube Dominique raia wa Kongo.
Kwa pamoja wakisomewa hati ya mashtaka na Wakili wa serikali, Kija Elias mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mmbando imeelezwa kuwa mnamo Septemba 03,2020 Katika maeneo ya Tegeta jijini Dar es Salaam walikutwa wameingia nchini bila kuwa na kibali wala kuwa na Visa ya kusafiria.
Mara baada ya kusomewa mashtaka yao wameshindwa kukidhi vigezo vya dhamana na wamerudishwa rumande.
Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 22, 2020 itakapotajwa tena.