×

Watano Mmbaroni Kwa Kuingia Nchini Bila Kibali

Watuhumiwa watano waliofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiwa chini ya jeshi la polisi wakipelekwa kusomewa mashtaka yanayowakabili.

 

Washtakiwa watatu raia wa Liberia na wengine  wawili raia wa Nigeria na Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili  yote yakiwa niya kuingia nchini bila kibali.

Washtakiwa hao ni Ibrahim Darbey (Liberia),Prince Robart (Liberia), Cream Milton (Liberia), Adewale Oyedeji (Nigeria) na Basube  Dominique raia wa Kongo.

Kwa pamoja wakisomewa hati ya mashtaka na Wakili wa serikali, Kija Elias mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mmbando imeelezwa kuwa mnamo Septemba 03,2020 Katika maeneo ya Tegeta jijini Dar es Salaam walikutwa wameingia nchini bila kuwa na kibali wala kuwa na Visa ya kusafiria.

Mara baada ya kusomewa mashtaka yao wameshindwa kukidhi vigezo vya dhamana na wamerudishwa rumande.
Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 22, 2020 itakapotajwa tena.

Leave a Comment