
JANA Ijumaa katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar historia nyingine katika jukwaa la burudani iliandikwa pale ambapo mafahari watatu wa Muziki wa Bongo Fleva, Alikiba, Diamond na Harmonize waliposhea jukwaa kwa kutoa burudani kwenye uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kampeni hizo zilizinduliwa jana kwa upande wa Dar pale wa Mkapa na kuhudhuriwa na viongozi, wasanii na wananchi mbalimbali, ambao walijitokeza kusikiliza sera za wagombe ubunge, udiwani na urais.

Kwa upande wa burudani kulipambwa na wasanii wengi, kama vile Harmonize, Alikiba na Diamond wateka shoo kwa MkapaIssa Liponda,Dar es SalaamMakomandoo, Madee, Maarifa, Snura, Dogo Janja na wengine wengi.
Kwa upande wa ile miamba mitatu ndani ya Bongo Fleva, jina la Harmonize lilikuwa la kwanza kuitwa jukwaani, kabla ya Kiba na Mondi, lakini kwa bahati mbaya, Konde hakuonekana jukwaani licha ya kukaa kwa zaidi ya dakika moja tangu alipoitwa kufanya shoo.
Ndipo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, akaamua kuwapandisha Manzese Music chini ya Madee na watoto wake, Dogo Janja na Maarifa ambao walipiga shoo kwa kupokezana vipaza sauti akianza Maarifa kisha Dogo Janja aliyekuja kumaliza mchongo.
Baada ya Manzese kufanya yao, ikaja zamu ya Konde Boy kufanya balaa lake na wakazi wenzake wa mitaa ya Temeke na Mbagala na maeneo Dar lakini safari hii akipanda bila gwanda wala kofia ya CCM jukwaani.Harmonize alianza na mkwaju wa Uno, Jeshi na kumaliza na Haujanikomoa.

Kisha ikaja zamu ya King wa Bongo Fleva, mmiliki wa mkwaju wa Mediocre, Alikiba akipanda jukwaani na Seduce Me, huku uwanja wote ukiimba naye pamoja. Kidela ikawa mkwaju wa pili kwa Kiba na ndiyo ambao ulimpandisha Abdu Kiba na hapo akaja akafunga na goma la Mediocre.
Diamond Platinumz, akafunga shoo hiyo ya wakubwa kwa kuichapa mikwaju mitatu ya kupasha moto misuli, akipanda jukwaani na mkwaju wa Baba Lao na kupokelewa na shangwe la umati wa watu. Mondi aliendeleza balaa lake kwa mikwaju ya Yope na kumaliza na goma la Timua Vumbi. Baada ya hapo mambo mengine yakaendelea kama yalivyopangwa.






