NYOTA wa Los Angeles Lakera ameibuka shujaa baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji wenye thamani zaidi katika fainali za ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa kwa kuifunga Miami Heat 4-2.
LeBron alitwaa tuzo ya MVP akiwa na timu tatu tofauti ikiwemo Miami Heat mwaka 2012& 2013, Cleveland Cavaliers mwaka 2016 na sasa Los Angeles Lakers.
Lakers ilishinda katika mchezo wao wa sita huku LeBron akifunga Triple Double ikiwa na maana ya kufunga pointi 28, mipira ya kurudi 11 na pasi ya usaidizi 10 katika mchezo huo.
Ushindi huo pia umewafanya Lakers kufikia rekodi ya Boston Celtics ya kutwaa mataji mengi ya NBA ambayo ni mara 17.
