×

Breaking: Mvua Kubwa Yaua Watu 12 Dar – Video

MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakary Kunenge, amesema kuwa mvua kubwa zilizonyesha juzi Jumanne, Oktoba 13, 2020 jijini humo zimesababisha athari kubwa ikiwemo vifo vya watu 12, ambapo wilaya ya Ilala ina vifo nane na Kinondoni vifo vinne.

Aidha, Kunenge amesema kuwa nyumba zaidi ya 800 zimeingiliwa na maji, huku nyumba 107 zimechukuliwa na maji na wananchi zaidi ya 480 wakipoteza makazi yao. Ameongeza kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na Kisutu, Chakula Bora, Tupendane, Barafu, Kisiwani na maeneo mengine.

“Kwa jumla jiji lote lilipata athari mbalimbali kutokana na mafuriko,” amesema  leo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake.

 

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaaam limesema limetoa taarifa pia kuwa limepokea taarifa za vifo vya watu 12 vilivyotokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo. Vifo hivyo vimetokea katika mkoa wa kipolisi Ilala na Kinondoni.

 

Leave a Comment