MTAYARISHAJI wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Tanzania, Producer S2Kizzy, ameeleza kuwa amevamiwa studioni kwake ya ‘Pluto World’ iliyopo Sinza-Lion jijini Dar es Salaam, kisha kupigwa na kufanyiwa uharibifu wa vifaa vyake na watu waliodai wao ni walinzi shirikishi.
S2Kizzy amefahamisha hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambapo ameandika kuwa: “Nimevamiwa studio, kupigwa na kufanyiwa uharibifu wa studio nzima, kuvunjiwa vifaa na vitu vya studio na hawa wanaodai wao ni ‘security’ na ulinzi shirikishi.
Studio kulikuwa na watu ambao walipigwa kama wezi, wanawake walidhalilishwa ikiwemo kuvuliwa nguo, kupigwa na kufanyiwa vitendo vya kinyama.
“Nimesikitisha na nimekatishwa sana tamaa, mimi kama kijana ambaye natafuta riziki, kazi zetu tunakesha na tunahangaika lakini mwisho wa siku tunavunjwa sana moyo na vitu ambavyo havina hivi ili wala lile,” ameongeza.
Mtandao huu ulimtafuta prodyuza huyo ili atolee ufafanuzi zaidi juu ya chanzo cha tukio hilo lakini kwa bahati mbaya hakupatikana.
