×

Kocha Mpya Yanga Tayari Safarini Kutua Dar


KOCHA  Cedric Kaze anayekuja kushika mikoba ya kuifundisha Yanga SC, yupo safarini kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuanza rasmi majukumu yake mapya.

Afisa Habari wa timu hiyo, Hassan Bumbuli, amethibitisha ujio wa Kocha huyo ambaye mapema leo alikuwa jijini Amsterdam, Uholanzi, kwa ajili ya kubadilisha ndege ya kumleta Tanzania.

Kaze anatarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa nne usiku leo kwa ndege ya Shirika la Ndege la KLM.

Leave a Comment