TUME ya Uchaguzi Visiwani Zanzibar (ZEC) imemtaka Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Kitaifa leo, Alhamisi, Oktoba 15, 2020, majira ya saa 7 mchana ili kujieleza.
Wito huo umekuja kufuatia malalamiko yaliyotolewa na Chama cha Demokrasi Makini kuhusu kauli aliyoitoa mgombea huyo siku za hivi karibuni akiwaambia wananchi wakapige kura Oktoba 27, mwaka huu, badala ya Oktoba 28, mwaka huu, siku iliyopangwa na ZEC.
Akizungumza baada ya kupokea wito huo, Mgombea huyo amesema…. “Narudia sote tukapige kura Oktoba 27.”
