KIONGOZI wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf ‘Mfalme’ amecharuka na kukataa kufokewa kwa kitendo chake cha kurejea kwenye muziki wa Taarab, baada ya kuukacha na kumrudia muumba wake kisha kwenda kuhiji Makka nchini Saudi Arabia.
Mfalme Mzee Yusuf amewarushia dogo hilo wanaoendelea kumjadili maisha yake na kusema, yeye ni mtu mzima na asingependa kupangiwa maisha yake.
“Sipendi kufokewa, mimi ni mtu mzima, ninaishi maisha yangu nijuavyo mwenyewe, wewe unayenifokea hunilishi wala hunivishi.“Ni nani alikwenda kwa Mwenyezi Mungu na kuambiwa yeye ndiye mkamilifu?
“Unaweza ukakuta mtu duniani anajifanya Mcha-Mungu sana, lakini pengine mwisho wa siku anayejifanya Mcha-Mungu, ndiye atakayeishia motoni na wasiotegemewa, ndiyo watakaingia peponi,” anasema Mzee na kusisitiza kuwa, hataki kufokewa ambapo pia ameahidi kuwatungia wimbo hao wanaomfokea.
Baada ya kukaa nje ya muziki miezi kadhaa, Mzee Yusuf alirejea kwenye kazi yake hiyo aliyoifanya tangu utotoni hadi sasa amekuwa mzee.
STORI: RICHARD BUKOS, DAR
