×

Dube Ajipa Majukumu Mapya Azam

MASHINE ya mabao ya Azam FC, Mzimbabwe Prince Dube amefunguka kuwa kwake siyo ishu kubwa katika suala la kufunga mabao kwani mipango yake akiwa uwanjani ni kuwatengenezea wenzake wafunge.

 

Straika huyo ameongeza kwamba kwake binafsi hakuna maana yoyote ile kwenye suala la kufunga mabao kutokana na kwamba amekuwa akipambana zaidi kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo ifanye vizuri katika Ligi Kuu Bara.Dube ndiye kinara wa ufungaji katika ligi kuu akiwa na mabao sita akifuatiwa na straika wa Simba, Meddie Kagere akiwa na mabao manne.

 

Dube amesema: “Jambo kubwa siyo mimi kufunga bali timu kushinda. Haitakuwa na maana yoyote kufunga halafu timu haijashinda, mara zote timu hutangulizwa mbele kwa sababu ndiyo tunayoipigania.

 

“Ikitokea nikafunga, nitashukuru lakini hata nisipofunga mimi nitamsaidia mwenzangu yeyote afunge ili timu ifunge kama ambavyo wenzangu wananisaidia mimi kufunga katika michezo iliyopita.

 

Katika hatua hii ukianza kufikiria ufungaji bora utakuwa unapoteza uelekeo mapema,” alisema Dube.

Stori: Said ally,Dar es Salaam

https://globalpublishers.co.tz/ligi-ya-mabingwa-kuendelea-leo-usiku-ajax-vs-liverpool/

Leave a Comment