
JIONI ya kesho Jumanne kwenye Uwanja wa Sokoine kutakuwa na mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Kocha Mkuu wa Mbeya City FC, Amri Said amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na anaamini watapata matokeo chanya.
“Yanga ni timu kubwa hivyo tutaingia kwenye mchezo huo tukiwa tunajua kuwa tunakutana na timu nzuri na yenye wachezaji wazuri, lakini tutapambana kadiri tuwezavyo,” alisema Said ambaye huu utakuwa mchezo wake wa kwanza wa ligi akiwa na Mbeya.
Derick Lwasye, Mbeya