KATIKA kuelekea mchezo wa leo Alhamisi katika Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze amewaondoa wachezaji wanne katika kikosi chake kitakachowavaa Polisi Tanzania akiwemo Carlos Fernandes ‘Carlinhos’.
Yanga inatarajiwa kuvaana na Polisi Tanzania saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar. Hicho ndiyo kitakuwa kibarua chake cha kwanza kocha huyo gumu kwa kuwa wana ulinzi mkali sana kule Kigamboni.
“Lakini kwa kuwa wapo hapa Dar basi naamini kuna watu watafanya kazi hiyo kwenye mchezo wao wa keshokutwa (leo) kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakati wakicheza na Polisi Tanzania na watamueleza kocha kile walichokiona.
“Labda hii ndiyo itakuwa nafasi yetu ya kufahamu kuwa wamebadilika kwa kiwango gani kabla hatujakwenda kwenye michezo mingine na baadaye mchezo wetu wa Novemba 7.
“Tunachofahamu tu mpaka sasa ndani ya siku tatu ni kwamba kocha wao anaweka mkazo kwenye safu ya ushambuliaji lakini bado hutajapata moja kwa moja anatumia staili gani,” kilisema chanzo hicho.
Yanga wanashika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 13 baada ya kucheza michezo mitano, wameshinda minne na kutoka sare mmoja.Simba wao wapo nafasi ya pili wakiwa wamepata matokeo sawa na Yanga lakini wakiwa na tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Wilbert Molandi na Careen Oscar, Dar.
