×

Cedric Kaze Aliamsha Yanga SC

KATIKA kuhakikisha wachezaji wake wanaongeza fi tinesi ya uwanjani, Kocha Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, amepiga marufuku ulaji wa chipsi mayai huku akiwataka kuanza kutumia lishe yenye virutubisho vya wanga.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kocha huyo akabidhiwe jukumu la kukinoa kikosi hicho akichukua mikoba ya Zlatko Krmpotic raia wa Serbia.

 

Kocha huyo amekaa na kikosi hicho tangu mwishoni mwa wiki iliyopita huko kambini Avic Town, Kigamboni jijini Dar akiwa anakiandaa kwa ajili ya mchezo wa leo Alhamisi wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, wachezaji hao wote wametakiwa kula vyakula aina ya wanga kama ugali wa dona na sembe, viazi vitamu, tambi, wali, ndizi, na vyakula vya baharini ‘Sea Food’.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, mfumo na aina ya soka la pasi analolitaka kocha huyo linahitaji wachezaji wenye fi tinesi ya kutosha, hivyo ni lazima wale vyakula vya wanga kwa ajili ya kuwaongezea nyota wake.

 

Aliongeza kuwa kocha huyo pia amebadili ratiba ya chakula cha mchana ambacho kila mchezaji anatakiwa awepo sehemu ya kula saa sita na nusu mchana badala ya saa saba na baada ya hapo wachezaji wote wanatakiwa kulala kwa ajili ya kupumzisha miili yao.

 

“Kocha Kaze ameonekana kuleta mabadiliko ya milo yote ya vyakula kwa wachezaji wake kwa kuhakikisha wanatumia lishe yenye virutubisho kidogo vya wanga.

“Kaze amewastopisha wachezaji kula chipsi mayai na vyakula vingine ambavyo siyo vya wanga, lengo ni kuhakikisha wachezaji wake wanakuwa na fi ziki ya kutosha wakiwa ndani ya uwanja.

 

“Pia amebadili ratiba ya chakula cha mchana kutoka saa saba hadi saa sita na nusu mchana ambapo wachezaji wote wanatakiwa kuwa kwenye meza ya chakula na amezuia matumizi ya simu kila muda huku akiwataka kutumia muda mwingi kulala kupumzisha miili yao,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Kaze kuzungumzia hilo, alisema: “Tarajia kuona mabadiliko mengi ndani ya timu mara baada ya mimi kuanza kazi ya kuifundisha Yanga, kikubwa ninataka kuona nidhamu na viwango vya wachezaji vinaongezeka katika timu.”

Leave a Comment