×

Global Yawapa Tuzo Wanafunzi Tumaini, UDSM

 

Nuhu Musa kutoka Turdaco akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya wenzake

UONGOZI wa Kampuni ya Global Publishers umetoa tuzo maalum kwa kundi la wanafunzi 30 kutoka katika Chuo Kikuu cha Tumaini na Chuo kikuu cha Dar es Salaam vitivo vya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma waliokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo baada ya kumaliza mafunzo yao katika Kampuni hiyo.

Tuzo hiyo imetolewa leo Alhamisi na Mhariri Mtendaji wa  Kampuni hiyo, Saleh Ally  ‘Saleh Jembe’ kwa wanafunzi  katika hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi hao waliodumu kwenye mafunzo yao kwa vitendo kwa muda wa wiki nane.

 

Baadhi ya waandishi na wahariri wa Global Publishers wakifuatilia hafla hivyo.

Jembe ametumia nafasi hiyo ya kuwaaga kwa kuwashukuru na kuwapongeza kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa katika mafunzo yao.

“Nitumie nafasi hii kuwapongeza wanafunzi wote wa ‘field’ waliopata nafasi ya kuja hapa Global kujifunza kiukweli mumenishangaza kwa utofauti mkubwa ambao mumeonyesha.

 

 

“Niwapongeze sana vijana wote, kiukweli mmefanya vizuri sana, uwezo wenu wa kubadilika kutokana na mazingira umekuwa wa hali ya juu sana.

 

“Nimepokea pongezi zenu juu ya namna ambavyo naweza kuwa rafiki na kiongozi kwa wakati mmoja, niseme hiyo ndiyo imekuwa tabia yangu na nitakufa nikiwa hivyo.

 

 

Mwandishi mwandamizi wa magazeti Pendwa Imelda Mtema, akiwapa neno wanafunzi hao.

 

“Lakini niwapongeze wafanyakazi wote wa Global Publishers kwa kuweza kuishi vizuri na nyinyi na kuwapa ushirikiano mkubwa, hii ndiyo asili yetu na tutakuwa hivyo siku zote.

 

Mkuu wa Kitengo cha Wasanifu Kurasa wa Global Publishers, Bahati Haule akitoa neno kwa wanafunzi hao.

 

“Nimeandaa hii tuzo kwa wanafunzi wa vyuo vyote, lakini kwa kuwa wale wa Tumaini wapo wengi, watapata nafasi ya upendeleo na wataondoka nayo hii tuzo ili ikawe kumbukumbu bora katika maisha yao ya chuo, kuwa tuliwahi kufanya ‘field’ Global na tukapewa hii tuzo kama ishara ya utendaji kazi mzuri.

 

 

 

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers Saleh Ally, akizungumza jambo mbele wa wafayakazi wa Global na wanafunzi hao waliokuwa wakiagwa leo katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar.

 

 

“Nimalize kwa kusema kuwa hapa ni nyumbani kwenu, mnakaribishwa wakati wowote mkihitaji kurudi. Ila ombi letu mkawe mabalozi wazuri huko muendako na kwa wale waliobahatika kupata nafasi ya kubaki, hakuna kulala ni mwendo wa kupiga kazi tu,” alisema  Jembe.

 

 

Saleh Ally akiwakabidhi tuzo ya heshima wawakilishi wa wanafunzi wa Chuo cha Tumaini University Dar es Salaam College Turdaco, Wlifred John kushoto na Glory Olomi kulia.

 

Baadhi ya wanafunzi hao wakifutahia pamoja na baadhi ya waandishi na wahariri wa Global Publishers baada ya hafla hiyo.

 

 

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Careen Oscar akiwa ameshika tuzo hiyo.

 

 

Baadhi ya wanafunzi na waandishi wa Global wakifurahia tuzo hiyo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Comment