×

Kamanda Muslim Aanika Chanzo cha Ajali ya Ngara

 

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim, leo Oktoba 26, 2020 amesema uchunguzi wa jeshi hilo umebaini kwamba ajali ya basi iliyotokea wilayani Ngara mkoani Kagera ilisababishwa na uzembe wa dereva na mwendo kasi.

 

Ajali hiyo iliyolihusisha basi la Kampuni ya Emirates lililokuwa likitokea Ngara kuelekea Bukoba, ilisababisha vifo vya watu 15 huku wengine 20 wakijeruhiwa.

Leave a Comment