×

Askofu Ruwa’ichi Aipongeza ACB Kuiwezesha Shule ya Mary Mother of Mercy

Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.

MHASHAMU Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Dar es Salaam, Jude Thadeus Ruwa’ichi ameipongeza Benki ya ACB na wadau wengine kwa kuiwezesha Shule ya Mary Mother of Mercy kwa kuwahifadhia fedha na kuikopesha hali iliyopelekea mafanikio makubwa iliyo nayo sasa.

Mhashamu Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar esb Salaam, Jude Thadeus Ruwa’ichi akizungumza kwenye uzinduzi na mahafali hayo.

Ruwachi alisema hayo kwenye uzinduzi wa shule hiyo iliyopo shule hiyo ya mtaala wa kiingereza iliyopo Gongo la Mboto, Mji Mpya, Jijini Dar ambapo alikuwa akiwasifu watu na taasisi mbalimbali zilizofanikisha maendeleo ya shule.

Mhashamu Askofu Mkuu, akimbariki mhitimu wa darasa la awali shuleni hapo.

Sambamba na uzinduzi rasmi wa shule hiyo kulikuwa na mahafali ya kwanza ya darasa la saba na darasa la awali.

Benki ya ACB kama wadau wa shule hiyo wamekuwa wakihifadhi pesa za shule hiyo pamoja na kuikopesa pesa kwa ajili ya maendeleo yake.

Meneja wa Benki ya ACB Tawi la Banana, Agnes Nyakali (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa benki hiyo, Innocent Ishengoma wakimpongeza mzazi wa Gerald Kyaruzi baada ya kuwaongoza wenzake kwenye mitihani ya kuhitimu darasa la saba kabla ya mtihani wa taifa.

Katika mahafali hayo benki hiyo ilimzawadia kiasi fulani cha pesa pamoja na kumfungulia akaunti mwanafunzi Gerald Kyaruzi ambaye aliwaongoza wenzake kwenye mitihani ya mwisho kuelekea mtihani wa taifa iliyofanywa shuleni hapo.

Meneja wa ACB Tawi la Banana, Agnes Nyakali akimkabidhi cheki mhitimu, Gerald Kyaruzi.

Meneja wa ACB Tawi la Banana Ukonga, Agnes Nyakali ndiye aliyemkabidhi kitita  mhitimu huyo kitita hicho na kisha kumfungulia akaunti kwenye benki hiyo akishuhudiwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko katika benki hiyo, Innocent Ishengoma pamoja na wageni waalikwa wengine. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave a Comment