
KAMPUNI ya simu, Infinix Mobility LTD inayotamba na toleo jipya aina ya Infinix HOT 10 imeendelea kuongeza mashabiki kupitia kampeni inayohusisha ushindani wa kurap #HOT 10 Rap Challenge. Akizungumzia simu hiyo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Aisha Karupa amesema simu hiyo inasifika kwa kukaa na chaji kwa muda mrefu (5200mAh) na sifa nyingine kama zilivyotajwa hapo chini;
- Media Tek Helio G70 Octa core processor
- 78 HD+ Infinity-O Display
- 5200 mAh battery
- 16MP Quad Camera
- 8MP Selfie Camera
- DTS Audio
Infinix wamekuwa wakifahamika kwa kuleta simu zinazokaa na chaji kwa muda mrefu na pia kushirikisha wasanii mbalimbali katika kampeni zao kupelekea mpaka kupata tuzo kutoka “Guinness World Record” ya video ndefu iliyoshirikisha wasanii mbalimbali kutoka nchi zaidi ya 50 duniani, akiwemo rappers Brian Simba na Eddy Super kutoka Tanzania, video hio ilifanyika kwanjia ya mitandao na rappers walionyesha ujuzi wao.

Bado wakaona haikutosha na kuleta mashindano ya mtandao ni maarufu kama “Online Challenge” iliyopata washiriki zaidi ya 100 katika mtandao wa Instagram wakiwania zawadi ya Infinix HOT 10 na fedha taslimu Tsh 300,000.
Joshua Joram ambaye ni mwanafunzi wa chuo ni mmoja wa wateja wa Infinix HOT 10, alisema, “Infinix wanajua kutupatia sana maana wanaleta simu zenye uwezo mkubwa kwa gharama nafuu ambazo hata mwanafunzi wa chuo anaweza kujibana mwenyewe tu na kununua sio kama brand nyingine,
Infinix HOT 10 imekuwa ni mkombozi kwasisi wanafunzi uwezo wake wa kudumu na chaji kwa muda mrefu pasipo na haja ya kuzima data inatusaidia sisi wanafunzi kujisomea mtandaoni lakini pia inatupa nafasi ya kuchangamsha akili na games mbalimbali kutokana na processor ya Media Tek Helio G70 kuweza kuhimili games zenye ujazo wa aina yoyote”.

Pamoja yakuwa ni simu pendwa kwa vijana wa kisasa lakini bado kampuni hiyo haijaacha tamaduni yake ya kufanya kampeni kwa njia ya promosheni ili kujiweka karibu zaidi na wateja wake na kwasasa ukitembelea duka lolote lenye promosheni ya Infinix HOT 10 tupo live basi pindi tu ununuapo bidhaa ya Infinix HOT 10 unapewa zawadi ya blenda, kinga’amuzi au headphone papohapo.
Infinix HOT 10 inapatikana katika maduka yote ya simu Tanzania kwa gharama isiyozidi Tsh 350,000 tembelea sasa ujipatie yako.