MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, na viongozi wenzake Godbless Lema na Boniface Jacob, wameachiwa kwa dhamana katika Kituo cha Polisi cha Oyster Bay jijini Dar baada ya kukamatwa juzi na polisi wa tuhuma za kuandaa maandamano kupinga mchakato wa matokeo ya uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti wa Chadema Kinondoni, Henry Kilewo, amethibitisha kuachiwa kwao.
