×

Chama Aibua Shangwe Simba

WAKATI kiungo wa Simba, Clatous Chama ikielezwa juzi hatokuwepo kwenye mchezo dhidi ya Yanga, mashabiki walilipuka shangwe baada ya kumuona akishuka kwenye gari la timu hiyo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi.

 

Chama ambaye aliumia katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar, huku kocha wa kikosi hicho, Sven Vandenbroeck akisema kwamba hataweza kucheza mechi ya juzi, upepo ulibadilika na kuanza kikosi cha kwanza.

 

Kiungo huyo raia wa Zambia, amekuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi hicho msimu huu ambapo kabla ya mechi ya juzi, alikuwa amefunga mabao mawili na kutoa asisti tano ndani ya Ligi Kuu Bara.

JOEL THOMAS NA CAREEN OSCAR

Leave a Comment