KWA mara ya kwanza, mchambuzi mahiri wa masuala ya soka, maarufu kama Mwalimu Kashasha, ametembelea ofisi za Global Group na kufanya mahojiano maalum na +255 Global Radio na Global TV Online, ambapo amezungumzia masuala mbalimbali ya soka yanayoendelea hapa nchini.
Miongoni mwa masuala aliyozungumza Mwalimu Kashasha ni haya:
“Jina la ualimu limekuja kwa kofia mbili, kwanza mwalimu wa mpira, pili nimefundisha kwenye levels mbalimbali za vyuo. Vyuoni nilikuwa nafundisha psychology, language na nyanja mbalimbali za michezo.
“Tunapaswa kujiuliza kwa nini timu hizi kubwa bado zina walimu kutoka nje wakati kila mara kuna kozi za makocha zinazotolewa na Fifa hapa nchini? Lakini hata hao wanaokuja wanatimuliwa. Hivi vitu natamani watu wajue kwamba tukiamini mpira ni sayansi, tutaweza.
“Mpira lazima uwe wa upinzani na wa kuvutia, game ya Simba na Yanga kila mmoja alikuwa bora kwa namna yake. Yanga kama kawaida yao waliingia kwa kucheza kwa kasi ili wapate bao na walifanikiwa, mwisho wa siku watu huuliza nani ameshinda siyo nani amepiga pasi nyingi.”


