×

Mhariri: King Kikii Anateseka, Tumsaidieni

MHARIRI wa gazeti hili la IJUMAA WIKIENDA, Sifael Paul anawaomba wapenzi na wadau wa burudani ya muziki nchini kumsaidia mwanamuziki mkongwe wa dansi, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’ kwa ajili ya matibabu kwani siyo siri anateseka.

 

King Kikii anapatiwa matibabu nyumbani kwake Temeke-Kwapile jijini Dar baada ya kufanyiwa upasuaji wa shingo. King Kiki alifanyiwa upasuaji huo takribani miezi mitatu iliyopita kufuatia kusagika kwa pingili tano za uti wa mgongo na bado hali yake haijatengamaa kwani sasa anasumbuliwa na tatizo la ganzi mwili mzima.

 

“Huyu mzee tumemsikia kwa miaka mingi akituburudisha hivyo tuna deni la kumjulia hali na tumsaidie kwa hali na mali kwani anapitia kipindi kigumu kwelikweli,” anasema Sifael. Kwa upande wake Constansia Kalanga ambaye ni mke wa King Kiki, naye amewasihi Watanzania na wapenzi wa muziki wa mumewe kumkumbuka kwa maombi bila kujali dini zao.

 

Amewaomba watakaoguswa kutoa msaada wa chochote kwa ajili ya kusaidia matibabu ya nguli huyo wa muziki Tanzania wanaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0713 311 673 King Kikii amesikika kwa zaidi ya miongo minne akitamba na nyimbo zake tamu kama Kitambaa Cheupe, Mtoto Kaanza Tambaa, Mtoto wa Mjini na nyingine nyingi.

STORI: MWANDISHI WETU, DAR

 

Leave a Comment