
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom PLC imezindua huduma ya Duka linalotembea ili kuwafikia wateja popote.
Uzinduzi umefanyika jana Jumatano katika Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom PLC, Linda Riwa amesema katika duka hilo zitapatikana huduma zote zinazopatikana kwenye maduka mengine ya Vodacom PLC.

Linda alizitaja huduma hizo kama vile kuuza simu na vifaa vyake, huduma za M-Pesa, usajili wa laini na mambo mengine.

Ameendelea kusema kuwa wameamua kufanya ubunifu huo kwa ajili ya kuwafikia kiukaribu wateja wao waliopo sehemu mbalimbali.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi walikata keki na kugonga shampeni pamoja na umati uliokusanyika eneo hilo kushangilia uzinduzi huo.