The House of Favourite Newspapers

Aliyemtishia maisha Kessy, afunguliwa mashtaka

0

Hassan-‘-Kessy’-Ramadhani2Hassani Kessy.

Wilbert Molandi,
Dar es Salaam
MENEJA wa beki wa pembeni wa Simba, Hassani Kessy, Tippo Athumani, yupo katika hatua za mwisho za kukutana na mwanasheria wao kwa ajili ya kumfungulia mashtaka mmoja wa mashabiki wa timu hiyo anayedaiwa kumtumia meseji za vitisho mchezaji huyo.
Hiyo ni siku chache tangu Kessy agomee mkataba wa kuichezea Simba huku tetesi zikienea kuwa beki huyo anawaniwa na watani wao wa jadi, Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Kuanzia Desemba, mwaka huu, beki huyo ataruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine inayomhitaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu kutokana na kubakiza miezi sita katika mkataba wake.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tippo alisema kuwa kwanza kabisa kabla ya kwenda kuripoti kituo cha polisi, amepanga kukutana na mwanasheria wao ili wapate mwongozo mzuri.
Tippo alisema, wanashangazwa na vitisho hivyo anavyopewa mchezaji wake ambavyo havina sababu ya msingi.
“Kila mtu ana uhuru wake wa kuamua jambo, kama yeye Kessy amegoma kuongeza mkataba, sasa kuna haja gani ya kupewa vitisho?
“Suala siyo dogo kama wanavyodhani hao mashabiki wenyewe, hivyo kama meneja wake tumepanga kulifikisha suala hilo mbele zaidi ikiwemo mahakamani ili sheria itende haki yake.
“Ushahidi wa meseji na namba hiyo tunayo,” alisema Tippo.

Leave A Reply