×

Kampuni ya Kulinda Wanafunzi KILA KONA Yaanza Kazi Dar

Mkurugenzi Mtendaji wa Kila Kona, Salim Rajab.

Kampuni ya Kidigitali ya Kuwalinda wanafunzi kila kona iitwayo KILA KONA imeanza kazi ya kuwalinda wanafunzi njiani wanapotoka nyumbani mpaka kufika darasani na hata mwanafunzi akichepuka na kukacha kuingia darasani.

Mwalimu wa shule ya Al Irshaad ambayo imeshaanza kutumia mfumo huo.

Akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar, leo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Salim Rajab amesema mfumo huo wa kuwalinda wanafunzi ndiyo suluhisho la usalama kwa mwanafunzi.

Akielezea mfumo huo unavyofanyakazi Salim amesema baada ya shule kujiunga mfumo huo kupitia kampuni yao mwanafunzi atapewa kadi ambayo itamuonesha popote aendepo kupitia simu au kompyuta ya mzazi au mlezi.

Mhandisi mitambo wa Kila Kona, Simon Lihundi, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari (hawapo pichani).

Mkurugenzi huyo amesema mpaka sasa wameshaanza kutoa huduma hiyo katika shule za Al Irshaad, Faraja Islamic, Mikocheni Islamic na nyinginezo ambazo bado wako katika mipango ya kuwaunganisha na huduma hiyo.

Naye mkurugenzi msaidizi wa kampuni ya KILA KONA, Ismail Juma  amewaomba wazazi kuutumia mfumo huo kwa ajili ya usalama wa watoto wao na kuacha kuishi kizamani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kila Kona, Salim Rajab akiwaelezea wadau waliofika kusikiliza ujio wa huduma hiyo mpya.

Kila jipya linapoingia linaingia lakini mhandisi wa mitambo wa kampuni hiyo…… amesema mfumo huo hauna usumbufu wa kama vile kukosekana kwa netiweki wala kumsumbua mtumiaji.

Mhandisi huyo ameendelea kusema kuwa katika mfumo huo kutakuwa na mambo mbalimbali kama vile maktaba, ratiba za masomo, vipindi vya michezo ya watoto na mambo mengine kwa ajili ya wanafunzi.

Muongoza matukio kwenye mkutano huo, Borry Mbaraka ambaye ni Meneja wa +255Globalradio akitoa muongozo. kwa wageni waalikwa. 

Mwalimu wa Shule ya Al Irshaad, Zena Kazikamwe ambaye shule yake imeshaanza kutumia mfumo huo ameelezea jinsi ulivyoanza kuwanufaisha kwa kuangalia kiurahisi mienendo ya wanafunzi wao. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave a Comment