×

Michuano Cecafa U20 Kuanza Novemba 22 Arusha

 

BARAZA la Michezo Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 itataanza kutimua vumbi Novemba 22 jijini Arusha.

Rais wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Wallace Karia, amesema michuano itashirikisha nchi tisa huku nchi mbili zikishindwa kushiriki.

Amesema michuano hiyo ilikuwa ifanyike Aprili mwaka huu nchini Sudan lakini kutokana na kuibuka homa ya mafua ya Corona (COVID 19) ilibidi kuahirishwa na ndiyo yataanza mwishoni mwa wiki hii.

Ameongeza kwamba michuano hiyo itakuwa na vituo viwili vya Arusha na Karatu huku timu zikigawanywa kwenye makundi matatu.

Timu zitakazoshiriki ni wenyeji Tanzania, Zanzibar, Somalia, Djibouti, Kenya, Uganda, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini huku Eritrea na Rwanda ndiyo pekee ambazo hazitashiriki.

Leave a Comment