
Kitabu hiki kimeandikwa na M.N Masala ili kumpa mwongozo wa vitendo msomaji juu ya namna ya kurejesha tumaini lililopotea. Dhamira ya kuandika kitabu hiki ni kuwainua wale wote walipoteza matumaini.
Ikumbukwe kuwa ”Mtu mwenye tumaini lililopotea, ni sawa na mwili mfu unaotembea”.
Kitabu hiki kimejikita zaidi kwenye maeneo yafuatayo:-
1. Kurejesha tumaini lililopotea katika uongozi bora kwa kutumia mwongozo wa vitendo wa Kanuni ya ISHINASISI;
2. Kurejesha tumaini lililopotea katika siasa kwa kutumia mwongozo wa kanuni ya TIJ;
3. Kurejesha tumaini lililopotea katika ujasiriamali kwa kutumia mwongozo wa vitendo wa sifa za mjasiriamali;
4. Kurejesha tumaini lililopotea katika muziki kwa kutumia mwongozo wa vitendo wa kanuni ya muziki;
5. Kurejesha tumaini lililopotea la kuwa mwajiliwa bora kwa kutumia mwongozo wa vitendo wa kanuni ya mwajiliwa mtiifu;
6. Kurejesha tumaini lililopotea katika uigizaji kwa kutumia mwongozo wa vitendo kutoka tasnia ya filamu;
7. Masomo ya kujifunza ili kukusaidia kutokukata tamaa;
8. Ushauri kwa mtu mmojammoja na kwa serikali.
Weka oda yako leo kupitia namba 0768 546 323.
