
NYOTA wa Kimataifa wa Simba akiwemo Clatous Chama na Meddie Kagere, leo Jumanne wanatarajia kurudi Tanzania na kujiunga na kikosi cha timu hiyo tayari kwa maandalizi ya michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika, inaanzia hatua ya awali kwa kucheza na Plateu United ya nchini Nigeria. Mechi ya kwanza itachezwa Nigeria kati ya Novemba 27-29, marudiano ni hapa Tanzania kati ya Desemba 4-6, mwaka huu.
Akizungumza na Spoti Xtra, Katibu wa Simba, Arnold Kashembe, amesema: “Maandalizi kwa ajili ya safari ya kikosi chetu yanakwenda vizuri. Nyota wetu wa kimataifa wote waliokuwa timu za taifa na wale waliokuwa na udhuru kwenda majumbani kwao wanatarajia kurudi kesho (leo) Jumanne tayari kwa kujiandaa na mechi za ligi pamoja na michuano ya kimataifa.”
KHADIJA MNGWAI, Dar