×

Uwoya: Ni Kweli Mimi ni Jini

STAA mwenye mvuto wa kipekee kunako Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya, amesema kuwa, watu wengi wanamfananisha na jini kutokana na uzuri alionao, lakini ukweli ni kwamba, kuna wakati mwingine akijitengeneza sura yake, anaonekana ni jini kabisa hivyo anakubaliana kabisa na watu wanaomuita jina hilo.

 

Hivi karibuni, Uwoya amepachikwa jina la jini kwenye mitandao ya kijamii kutokana na namna anavyojipodoa, kiasi cha kuwa na mwonekano wa viumbe aina ya majini.

 

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Uwoya anasema kuwa, kuna mtu anaweza kumwambia mtu ni mrembo na anavutia, lakini asiuone huo urembo wake moja kwa moja, ila kwa upande wake yeye anajiona kabisa ana mvuto wa hatari.

 

Katika hali hiyo, Uwoya anasema kuwa, anamshukuru mno Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia baraka hiyo ya kipekee kwani ni wanawake wachache wanaokuwa nayo.

 

“Kuna wakati mwingine ninajiangalia kwenye kioo, ninajiona kweli mimi ni jini kabisa maana kuna wakati ninakuwa mzuri mpaka ninapitiliza,” anasema Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Krish.

 

Stori: Imelda Mtema

Leave a Comment