×

Vodacom Kugawa Zawadi za Kusisimua Kusherehekea Miaka 20

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni akizungumza kwenye uzinduzi huo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania PLC Linda Riwa.

DAR ES SALAAM, jana Novemba 21 Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali, Vodacom Tanzania PLC imeendelea kusherehekea miaka ishirini ya utoaji huduma tangu ilipoanza kufanya kazi hapa nchini Tanzania. Katika kipindi hiki, kampuni hiyo imeongoza kuleta mabadiliko katika mifumo ya mawasiliano ya simu, mfumo wa malipo, na hivyo kubadilisha maisha ya mamilioni ya Watanzania.

Ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20, Vodacom Tanzania PLC leo imezindua kampeni ya msimu wa sikukuu ijulikanayo kama”Shangwe Shangwena” ambapo kupitia kampeni hii, Vodacom itawazawadia wateja wake ambao wamejikita zaidi katika mtindo wa maisha wa kidijitali kwa kutumia mfumo wa malipo ya kijanja wa M-Pesa.

Wakiwa na picha yenye mfano wa magari hayo.

Wateja hawa zaidi ya 15 milioni, watajishindia zawadi zenye thamani ya Shilingi 3 Bilioni zikiwemo magari mapya 5, zawadi za pesa taslim,rejesho la fedha pindi mteja anapolipia bidhaa au kutuma hela  kupitia M-Pesa, MB za bure, muda wa maongezi, jumbe fupi (SMS) pamoja  na punguzo la bei pindi mtejaanapofanya manunuzi ya simu janja kwa kutumia M-Pesa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania PLC Linda Riwa alisema kwamba anajivunia hatua ambayo Vodacom imefikia katika miaka ishirini iliyopita kwa kukuza maisha ya kidijitali nchini.

Wakurugenzi hao wakiingia ndani ya moja ya magari hayo kuiangalia ubora wake.

“Maono yetu ya kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa kidijitali kupitia teknolojia sasa yanathibitika, kwani ubunifu wa bidhaa na huduma zetu umeleta matokeo chanya kwenyejamii kwa mfano mfumo wa malipoya M-Pesa, suluhisho kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kupitia Lipa kwa Simu, mikopo kupitia M-Pawa na Songesha, Vodacom imebadilika kutoka kampuni ya mawasiliano tu na kuwa mwezeshaji wa maendeleo ya kiuchumi katika jamii,” alisema Bi Riwa.

Kampeni ya Shangwe Shangwena itawazawadia watejazawadi mbalimbali na ofa maalum, zitakazowawezesha kufurahia huduma za mawasiliano wakati huu wa msimu wa sikukuu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni aliwashukuru wateja kwa uaminifu wao kwa miaka 20, na pia kwa kupokea maendeleo ya kiteknolojia na kusema kuwa msimu huu kampuni hyo inataka kusherehekea pamoja na wateja wake kupitia kampeni hii ya Shangwe shangwena.

Gari likisubiri mshindi.

“Wateja wanapata nafasi ya kushinda, wakati wowote wanapotumia huduma za M-Pesa kwa kufanya moja au yote kati ya haya; kufanya miamala ya fedha kati ya mtu na mtu (P2P), malipo ya biashara kupitia Lipa kwa Simu, Kuhamisha pesa kutoka Benki kwenda M-Pesa (B2C), Malipo ya huduma kama vile Luku, Dawasco nk, pamoja na ununuzi wa vifurushi, muda wa maongezi na simu janja au vifaa vya simu,” aliongeza Mbeteni.

Shangwe za uzinduzi zilikuwa kama zote.

Mbeteni aliwahimiza wateja kuendelea kutumia huduma tofauti za kidijitali kutoka Vodacom ili wajiongezee nafasi ya kushinda zawadi kemkem na za kufurahisha zinazotolewa wakati wa msimu huu  wa sikukuu.

Leave a Comment