Makamu wa Rais Samia Ashiriki Mbio za NBC Marathon Dodoma
Global Publishers November 22, 2020 0 Comments
SHARE THIS:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi mfano wa Hudi ya Shilingi milioni mia moja 100,000,000. Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaitenanga iliyotolewa na Banki ya NBC kwa ajili ya kuchangia mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama kwenye Maadhimisho ya Mashindano NBC Marathon mwaka 2020 yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama yaliyofanyika leo Novemba 22,2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan leo Novemba 22, 2020 ameshiriki katika mbio za NBC Marathon zilizofanyika Jijini Dodoma ambapo alikuwa mgeni Rasmi.
Viongozi mbalimbali wa Serikali pia walishiriki mbio hizo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza mashindano ya NBC Marathon Mwaka 2020 leo Novemba 22,2020 Jijini Dodoma yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama. Mashinda.
Akihutbia mara baada ya mashindano hayo Makamu wa Rais amesema anaamini kuwa wanariadha wa nje wamevutika kushiriki Marathon hii kwa sababu ina utambuzi wa Kimataifa kama na viwango hivi vya Kimataifa vya mbio hizi ni jukwaa zuri la wanariadha wetu kujifua kwa ajili ya mashindano ya Olympics na Jumuiya ya Madola.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa kwenye maadhimisho ya mashindano ya NBC Marathon Mwaka 2020 yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama yaliyofanyika leo Novemba 22,2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
“Ni matarajio yetu kwamba wanariadha hawa wa nje wameongeza ushindani na hivyo kuongeza ubora wa mbio hizi lakini pia kukutana kwenu leo iwe ni mwanzo wa kujuana na kujenga udugu na mshikamano” ameongeza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimvisha Medali mshindi wa kwanza wa mashindano ya NBC Marathon Mwaka 2020 kilomita 42 Philipo Kipingu kutoka Uganda baada ya kushinda mashindano hayo yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama. Mashindano hayo yamefanyika leo Novemba 22,2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Aidha Makamu wa Rais amepoingeza lengo la mashindanohayoya riadha kwani kiasi cha shilingi 75 milioni zitakazokusanywa zitaelekezwa katika vita dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya uzazi kupitia Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI).
“Benki ya NBC ndiyo benki kongwe hapa nchini yenye miaka zaidi ya 50. Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limezaliwa mwaka 1954, wakati huo ikiitwa Tanzania Athletics Association (TAA), hivyo mashirikiano yanayooneshwa kati ya taasisi hizi mbili kongwe ni jambo la faraja. Ni matumaini yangu kwamba, ushirikiano huu utazaa mambo makubwa zaidi kwenye sekta yetu ya Riadha.”
Makubaliano ya ushirikiano ni kwa kipindi cha miaka mitano ambapo NBC itawekeza jumla ya milioni 300 kwa RT ili kukuza mchezo wa riadha nchini hasa katika mchezo wa mbio ndefu. Aidha, kutokana na mapato hayo RT itaweza kuwahudumia na kuwaandaa wanariadha waliofuzu kushiriki katika mashindano makubwa ya riadha kama vile Olimpiki, Jumuiya ya Madola, Mashindano ya Dunia na Mashindano ya Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi fedha taslim mshindi wa kwanza wa mashindano ya NBC Marathon Mwaka 2020 kilomita 42 Wanawake Muruki Muruki kutoka Kenya baada ya kushinda mashindano hayo yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano zidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama. Mashindano hayo yamefanyika leo Novemba 22,2020 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.