
NICOLAS SARKOZY, rais wa zamani wa #Ufaransa anayetuhumiwa kujaribu kutoa hongo kwa jaji na kupelekea ushawishi kwenye kampeni za mwaka 2007 atafikishwa mahakamani leo.
Sarkozy aliyeongoza Ufaransa mwaka 2007 hadi 2012 amekanusha makosa yote dhidi yake na anapambana vikali ili kesi hizo zifutwe.
Wachunguzi walikuwa wakisikiliza mazungumzo kati ya Rais Sarkozy na Wakili wake, Thierry Herzog, walipokuwa wakichunguza madai ya ufadhili wa Libya.
Uchunguzi uligundua Sarkozy na wakili wake walikuwa wakiwasiliana kwa kutumia simu za mkononi zilizosajiliwa kwa majina ya uongo.