×

Shigella Awasimamisha Kazi Watumishi TRA,TBS

                                                     Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella

MKUU wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella, amewasimamisha kazi maofisa wanane wa taasisi tatu tofauti, ikiwemo TRA, TBS na idara ya mifugo katika kituo cha forodha kilichopo mpaka wa Horohoro kwa madai ya kujihusisha na rushwa  na kuisababishia serikali hasara.

 

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara waliyoyatoa kwa kwake kuwa vitendo vya rushwa vimekithiri katika ofisi za watumishi wa serikali katika mpaka huo, na ndipo alipoamua kuunda kamati maalumu ya uchunguzi iliyoanza kazi yake Novemba 18 kwa ajili ya kuchunguza mwenendo wa watumishi hao.

 

Hapa wamegeuza kuwa ni shamba la bibi, hawa wanaenda kwenye taratibu za kiuchunguzi na vyombo vya dola viwachukue wakaanze kutoa maelezo kwa nini wasipelekwe mahakamani, na hapa waletwe watumishi wengine.  Tunataka kituo cha Horohoro kiwe cha mfano kwa kuhudumia wateja,” amesema  Shigella.

Leave a Comment