Usiku wa kuamkia leo ulikuwa ni kama ‘zari’ kwa Wabongo pale Bondia Mtanzania, Salim Mtango alipomchakaza bondia wa kimataifa kutoka Ufilipino, Eduardo Mancito, muda mfupi kabla ya Bondia Iddi Pialali kumchapa Bondia wa Kimataifa, Arnel Tinampay naye kutoka Ufilipino katika pambano la raundi nane.
Mtango na Mancito ndiyo walioanza kucheza pambano la utangulizi akitetea mkanda wake wa UBO uliokuwa ukiwaniwa na Mfilipino huyo.

Hata hivyo baada ya kuupata mkanda huo, Mfilipino huyo aliambulia kipigo na mkanda huo kuendelea kubaki hapa nchini ukishikiliwa na Mtango.


Mtango akimpelekea Mancito konde la uso.
