×

Pialali, Mtango Waishukuru Global Publishers

Meneja wa Global Publishers Abdalah Mrisho (kushoto) akisalimiana na bondia Iddi Pialali (aliyevaa miwani) walipotembelea Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori Dar, leo Desemba 1, 2020.

  

MABONDIA wa ngumi za kulipwa waliokuwa na mapambano ya kimataifa Novemba 28, mwaka huu, Idd Pialali na Salim Mtango, leo Desemba Mosi wametembelea ofisi za kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti ya Championi,  Spoti Xtra, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Uwazi kwa ajili ya kutoa shukrani kutokana na sapoti kubwa waliyoipata katika kufanikisha mapambano yao.

 

Mabondia hao wote wawili walishinda kwa pointi mapambano yao yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Next Door Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo, Pialali alimshinda Mfilipino, Arnel Tinampay, huku Mtango akishinda dhidi ya Eduardo Mancito.

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Global Publishers, Saleh Ally (kulia), akisalimiana na mabondia Idd Pialali na Salim Mtango walimpotembelea ofisini kwake.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Pialali alisema: “Napenda kuwashukuru wale wote waliofanya kazi kubwa ya kufanikisha pambano dhidi ya Tinampay.

 

“Kwa namna ya pekee namshukuru Promota Kapteni Selemani Semunyu na kampuni ya Global Publishers kwa mchango mkubwa mpaka kufanikisha mapambano hayo.”

Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa wa Global Pulishers, Richard Manyota (kulia) akiongea jambo na mabondia hao.

Kwa upande wake, Mtango alisema: “Tunawashukuru wadau wote waliopambana kufanikisha mapambano yetu, hatuwezi kuwataja mmoja-mmoja lakini ni wazi walifanya kazi kubwa,”

 

Mabondia wengine walioambata nao ni, Selemani Kidunda, Ismail Galiatano na  Adam Kipenga.

 

 

Msanii wa vichesho, Mkali Wenu, aliyebeba mikanda akiwa kwenye picha ya pamoja na mabondia Selemani Kidunda, Ismail Galiatano na  Adam Kipenga..

Stori na Joel Thomas

Leave a Comment