
MUDA mfupi baada ya Harmonize kushea picha na ujumbe wa kumtambulisha mtoto wake wa kike, Zulekha Kondegir,l aliyempata na mwanamke mwingine, mkewe, Sarah Michelloti, amemjibu kwa kusema Harmonize amejipa mtoto ambaye siYo wake.
Kupitia ukurasa wake Instagram, Sarah ameandika kuwa”Mungu wangu watu kweli wamevurugwa, mara mbili wamepima DNA ya mtoto bado majibu ni Negative, ila kwa kuwa umeshindwa kupata mtoto umeamua kujipa mtoto asie wako”

“Hongera kwa adoption, utakua na roho nzuri hukujua jinsi ya kutunza mke sababu ya maovu yako natumai utajua kutunza mtoto, ukome kuongopea mashabiki dah, nimepost hii kwa lugha ya kiswahili kila mtu ataelewa”.