KAMPUNI ya GSM imetangaza habari njema kwa wateja wote watakaotembelea na kufanya manunuzi kwenye maduka yao yaliyopo Mlimani City Dar, Nyerere Road, Msasani Mall na Duka lao lililopo Dodoma ambalo linatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni. Akizungumza na Wanahabari kwenye duka lao lililopo Mlimani City Dar, Afisa Biashara Mkuu wa GSM Group of Companies, Allain Kichonjo amesema promosheni ambayo imeshaanza desemba hii nitakwenda mpaka mwishoni mwa januari mwakani.

Kichonjo amesema wateja wote watakaotembelea maduka hayo na kufanya manunuzi watapata nafasi ya kuingia kwenye droo ambayo itawawezesha kujishindia zawadi ya pesa taslimu, kupambiwa nyumba kisasa kabisa kwa kutumia fenicha zao, kujishindia safari ya kutembelea hifadhi ya Ngorongoro na zawadi nyinginezo.

Kichonjo amesema mteja atakayejishindia safari ya kwenda kutalii hifadhi ya Ngorongoro atapata ofa ya kwenda na mpenzi wake na kugharamiwa kila kitu na kampuni hiyo akiwa kwenye safari hiyo.
Maduka ya GSM yamejizolea umaarufu kwa uuzaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo fenicha, vyombo vya ndani, mavazi na nyinginezo.

Kichonjo amesema pamoja na zawadi hizo pia wateja hao wanaweza kujishindia zawadi ya kitanda cha kisasa kabisa. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL