
Kauli ya mama yake Abigail ilimpa nguvu Felix kwani siku iliyofuata alianza kumtafuta msaidizi maalumu ambaye angemuhudumia Abigail baada ya kufunga ndoa. Baada ya siku tatu, mambo hayakuwa kama Felix alivyotarajia.
Wazazi wa Abigail walikataa suala la ndoa kwa sababu binti yao hakuwa na kumbu kumbu yoyote walihofia huenda baadae ingeleta shida baada ya kumbu kumbu kumrejea.
Felix hakukata tamaa aliwabembeleza wazazi wamruhusu basi amchukue akaishi nae nyumbani kwake huku akiendelea na matibabu kwani hakupenda kuendelea na zile safari za kwenda kwao Abigail kumjulia hali kila siku aliona ni bora awe nae nyumbani kwake. Kwa kuwa Felix alikuwa kijana mwenye uwezo mkubwa kifedha na aliemiliki jumba na magari ya kifahari, hii iliwafanya wazazi wake Abigail kutomtilia shaka hata kidogo.
Waliamini asingeshindwa kumuhudumia mtoto wao. Walikubali amchukue aishi nae lakini asifunge nae ndoa mpaka atakapopona vizuri na kurejea katika hali yake. Felix alifurahi sana, “Wazazi wangu nawashukuru sana! sana! nawaahidi kumtunza na kumpa uangalizi wa karibu sana binti yenu kwani nampenda sana!” Aliongea Felix huku akifunga mlango wa gari yake tayari kwa kuondoka.
Maisha mapya kati ya Felix na Abigail yalianza wakiwa ndani ya jumba la kifahari mahali ambapo Abigail alipata kila kitu alichokihitaji. “Binti, huyu ni mke wangu mtarajiwa, ninampenda sana.
Hapa alipo hawezi kuongea chochote yupo tu, yeye ni kutazama na kucheka. Sasa naomba umwangalie na kumuhudumia kwa ukaribu zaidi. Nimekuleta hapa kwa ajili hiyo tu. Hizi kazi zingine waachie hawa uliowakuta sawa!” Aliongea Felix akitoa maelekezo kwa binti Veronica ambae alimleta kwa ajili ya kumuhudumia Abigail.
“Usijali shemeji nitafanya kama unavyotaka ondoa shaka kabisa mbona wewe mwenyewe utafurahi,” alijibu Veronica huku akionyesha tabasamu usoni mwake.
Siku iliyofuata Veronica aliamka asubuhi sana na kuwaandaa watoto waende shule. Watoto hao walikuwa ni Elizabeth na mtoto wake wa kiume aliyeitwa jina sawa na aliyekuwa mpenzi wake Abigail wa mwanzo yaani Jonathan. “Jonathan fanya haraka baba! si unaona mwenzako Elizabeth amemaliza chai yake bado wewe,” Veronica alisikika akizungumza na watoto. “Aaam! hivi huyu mtoto wako anaitwa Jonathan pia?”
Felix alimuuliza Veronica huku akitokea chumbani kwake kuelekea sebuleni alipokuwa ameketi Veronica na wale watoto. “Ndio shemeji kwani kuna tatizo?” Alijibu Veronica.
“Hapana hakuna tatizo nimeshangaa tu kwani kuna mtu maarufu sana niliyewahi kukutana nae aliitwa Jonathan pia,” hata kabla Felix hajamaliza kuelezea, Elizabeth alidakia.
“Hapana dada hilo ni jina la baba yangu aliitwa Jonathan lakini amefariki tayari!” Elizabeth alimalizia kuongea huku machozi yakimlenga ndani ya mboni za macho yake.
Felix alipigwa na butwaa na kuonyesha hali ya kuvurugwa hivi.
“Wewe mtoto baba yako yupi unaemsema? Mimi si ndiye baba yako? Jonathan hakuwa baba yako,” Felix alijitahidi kutoa maelezo lakini mtoto Elizabeth hakumuelewa hata kidogo alizidi kulia.
Veronica alikuwa kimya akiyasikiliza mazungumzo yao huku maswali mengi yasiyo na majibu yakizidi kupita ndani ya ubongo wake.
Alinyanyuka na kumbembeleza Elizabeth na kisha kumwambia Felix, “Shemeji inaonekana kuna shida hapa. Naomba nimalizie kuwaandaa watoto kwani baada ya kuja huku, shule ya Jonathan imekuwa mbali zaidi,” Felix aliondoka na kurudi chumbani kwake pasipo kuzungumza neno lolote.
Veronica alimpeleka mwanae shule huku Elizabeth akifuatwa na gari la shule. Baada ya kurejea nyumbani, alianza kutoa huduma kwa Abigail. Alianza kwa kumfanyia mazoezi ya viungo kisha alimuogesha na kumpamba kwa mavazi mazuri.
Akiendelea na zoezi hilo, ilisikika sauti ya mtu akibisha hodi katika mlango wa chumba hicho. “Karibu pita ndani,” alijibu Veronica. Mlango ulifunguliwa na alikuwa ni Felix.
Veronica alinyanyuka haraka na kuchukua kitenge kilichokuwa kwenye sofa na kisha alijifunga. “Mbona umeshituka hivyo! Hapana kaa hivyo hivyo umependeza na khanga yako moja kwanini uongeze nguo nyingine juu?” aliongea Felix huku akimnyang’anya kile kitenge.
Felix aliongea vile bila wasi wasi yoyote kuwa Abigail angemsikia kwani alikuwa katika usingizi mzito baada ya kumeza vidonge ambavyo mara nyingi alisinzia usingizi mzito baada ya kuvimeza.
Felix alianza kumsifia Veronica kwa umbile lake zuri na macho ya kuvutia. Veronica hakupendezwa na tabia hiyo aliyoionyesha Felix.
“Samahani shemeji naomba nikupishe kidogo umsalimie mke wako,” alijibu Veronica huku akielekea mlangoni kutoka nje ya chumba. Macho yake Felix yaliyatazama makalio makubwa ya Veronica huku akitabasamu kwa mbali. Siku hiyo ikawa mwanzo wa Felix kujenga mazoea ya karibu na Veronica.
Alizoea kuondoka nyumbani mapema na kurudi amechelewa sana lakini baada ya kumshuhudia Veronica ndani ya khanga moja, aliibadili ratiba yake na kuanza kurudi nyumbani mapema sana jambo ambalo lilimshangaza sana Veronica.
Siku moja usiku muda wa saa nane kila mmoja katika nyumba ya Felix akiwa amelala, Felix alitoka katika chumba chake na kuelekea chumbani kwa Veronica.
Alinyata kiasi cha kutosikika na mtu yeyote na taratibu aliukaribia mlango wa chumbani na kukinyonga kitasa kisha alifanikisha kuingia chumbani. Hakuamini alichokiona baada ya kutupia macho yake kitandani na kumshuhudia Veronica akiwa amelala kifudifudi huku akiwa amevalia nguo ya ndani tu.
Alijikuta akijitupia kitandani na kujilaza pembeni ya Veronica. Felix alianza kumpapasa makalio yake makubwa na kumbusu katika lipsi zake. Veronica alishituka kutoka usingizini na kupiga kelele kiasi cha kusikika nyumba nzima. Felix alimziba mdomo na kumwambia kwa sauti ya chini.
“Usipige kelele Vero mimi ni Felix kuwa na amani,” aliongea Felix huku mkono wake wa kushoto akiupitisha taratibu katikati ya mapaja ya Veronica kitendo kilichomfaya Veronica alegee na kuacha kupiga kelele.
Felix aliendelea kumshika maeneo nyeti ya mwili wake na hiyo kumpelekea Veronica kukosa neno lolote na kuanza kutoa sauti za mahaba zilizomvutia zaidi Felix na kujikuta akitoa nguo yake ya ndani na kisha kutoa ya Veronica. Hakika ulikuwa ni usiku ambao wawili hawa walijihisi wapo katika ulimwengu mwingine.
Felix alimuonyesha ufundi wote Veronica kitendo kilichomfanya Veronica kushindwa kukataa na kuendelea kuzama katika penzi la kijana Felix.
Alfajiri iliwadia kila mmoja akiwa mchovu kutokana na shughuli waliyoifanya usiku ule na huo ndiyo ukawa mwanzo wa penzi jipya kati ya Felix na Veronica. Kama kawaida Veronica aliianza ratiba yake ya kuwaandaa watoto ili waende shule.
Akiwa sebuleni anawapatia kifungua kinywa watoto, Felix alitokea huku akionyesha tabasamu murua usoni pake na kumkonyeza Veronica. “Mama Jonathan acha hao watoto nifate mara moja,” aliongea Felix.
Wawili hawa walielekea katika chumba ambacho mara nyingi kilitumika kama kuna wageni nyumbani hapo. Waliketi katika masofa na Felix alivishika viganja vya mikono ya Veronica kana kwamba alitaka kumueleza jambo.
Kabla Felix hajanena neno lolote kwa Veronica, ilisikika sauti ya mtoto wa Veronica. “Maamaa…njoo haraka anti kaangukaa.” sauti ile ilipenya masikioni mwa Veronica na kumfanya akimbie kutoka pale alipokuwa ameketi na Felix kuelekea chumbani alipokuwa amelala Abigail.
Ni kweli Abigail alikuwa ameanguka chini kutoka kitandani alipokuwa amelala na kwa bahati mbaya zaidi, aliangukia kipande cha kioo ambacho Veronica alipenda sana kukitumia.
Kipande hicho kilimchoma Abigail usoni na kupelekea jeraha kubwa lililoruhusu damu nyingi kuchuruzika. Furaha ya Felix iligeuka kuwa majonzi badala ya kwenda kazini asubuhi ile, ilimbidi amkimbize Abigail hospitalini.
Baada ya matibabu, walirejea nyumbani. Felix hakuona sababu ya kuendelea na mazungumzo kati yake na Veronica. Alijiandaa na kuelekea kazini japo mawazo yote yalikuwa kwa binti Veronica.
Heri Niwe Peke Yangu – 05
******************ITAENDELEA*********************
Jalia Yusuph
Simu: 0622 216 238woman
@kalamu_na_karatasi