
KOCHA Jose Mourinho wa Tottenham sasa ameanza kutamba baada ya timu yake kuonekana inaweza kushindania ubingwa msimu huu, katika Premier League.
Bosi huyo wa Spurs aliiongoza timu yake mbele ya mashabiki 2,000 kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal, juzi usiku, matokeo ambayo yamewafanya wawe katika nafasi nzuri kwenye mbio za ubingwa huo.
Mourinho amesema: “Tumekua, watu wengi wanaweza kufikiria mechi tatu ngumu tulizocheza mfululizo dhidi ya Manchester City, Chelsea na Arsenal kwamba ulikuwa ni wakati wetu wa kupoteza pointi na kurejea kwenye nafasi ya kuwa timu ya kawaida.
“Lakini hatujarejea kule walikokuwa wakifikiria, tuko hapa na tutaendelea kuwa hapa.”
Son Heung-min alifunga bao la kwanza kwa shuti kali kisha nahodha wa timu hiyo, Harry Kane akapigilia msumari wa mwisho.“Wachezaji wangu wanafanya kazi kama wanyama, nawaheshimu wanyama, msije mkanifikiria vibaya, wanafanya kazi nzuri hata kama wakiwa hawana mpira.Bao la Kane lilikuwa la 250 katika maisha yake ya soka, ambapo ni bao la 100 akiwa nyumbani akiichezea Spurs na la 11 dhidi ya Arsenal