
Polisi nchini Uingereza wanachunguza madai ya shambulio baada ya staa wa Manchester United Cristiano Ronaldo kuonekana akivunja simu ya shabiki mmoja.
Ronaldo baadaye aliomba msamaha baada ya video inayomuonyesha akivunja simu ya shabiki huyo kusambaa
Picha zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii wakati akitoka nje ya uwanja baada ya timu yake kupoteza mechi dhidi ya Everton 1-0, Ronaldo, 37, baadaye aliingia kwenye mitandao ya kijamii na kuomba msamaha
“Si rahisi kukabiliana na mihemko katika nyakati ngumu kama ile inayotukabili,” alisema.
“Hata hivyo, kila mara tunapaswa kuwa na heshima, subira na kuwa mfano mwema kwa vijana wote wanaopenda mchezo huo mzuri,” Mreno huyo aliongeza.
“Ningependa kuomba radhi kwa hasira yangu na, ikiwezekana, ningependa kumwalika shabiki huyu kutazama mchezo huko Old Trafford kama ishara ya mchezo wa haki na uanamichezo.”