×

Asimulia Anavyokung’utwa Kisa Michepuko ya Mumewe!

DAKTARI mmoja mwanamke nchini Nigeria ameibuka hadharani na kutoboa ukweli ya yanayotokea ndani ya ndoa yake kupitia manyanyaso mengi na ukatili unaotishia uhai wake toka kwa mumewe huyo.

 

Mama huyo ambaye ni daktari wa magonjwa ya binadamu (jina lake limehifadhiwa) amesema kwa miaka mingi mumewe huyo amekuwa akiendekeza vitendo vya umalaya vya kubadilisha wanawake kila mara huku akimnyanyasa mkewe huyo kwa vipigo na kuamua kuvumilia ndoa isivunjike labda mwanaume angebadilika.

 

Anasema kilichomzindua sasa aanze kunusuru maisha yake ni kwamba, ana wiki nne tu tangu ajifungue mtoto wao wa nne kwa oparesheni lakini licha ya mshono alionao anasema mume hakujali alianza kumpiga.

 

Ameeleza kuwa sababu ya kumpiga  mke huyo ni baada ya kumweleza mumewe kuwa kwa sasa tayari wana watoto wanne, hivyo ni vyema baba huyo  akawa na matumizi mazuri ya pesa badala ya pesa anazopata kuishia kwenda kuzitumia kwa michepuko yake anayobadilisha kila wakati, maneno ambayo yalimuudhi mwanaume huyo  na kuanza kumshushia kichapo cha kufa mtu.

 

Mwanadada huyo ambaye ameishi kwenye ndoa na mumewe huyo kwa miaka  mingi na kubahatika kupata watoto wanne, amesema mimba ilipokuwa na miezi mitatu alipigwa na mume huku akimkalia tumboni.

 

Mume huyo aneyeitwa Pius anafanya kazi kwenye Kituo cha Channels TV na tayari mwajiri wake ameagiza uchunguzi ufanyike baada ya video ya mkewe kuhusu manyanyaso hayo  kusambaa.

Leave a Comment